Mkuregenzi Mtendaji wa Wild Frontiers, ambaye ndio muandaaji wa mbio hizo, John Addison alisema usajili wa mwaka huu umeongezeka kutokana na kuongezeka kwa mitandao ya kijamii hivi kurahisisha usajili.
“Wingi wa mitandao ya kijamii umesababisha ongezeko hili kwani usajili umeongezeka kwa asilimia 100 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu nah ii ni dalili nzuri kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi,” alisema huku akisema mbio za mwaka jana zilishirikisha wanariadha zaidi ya 7000.
Usajili utafanyika katika hoteli ya Kibo Palace Arusha Februari 25 mwaka huu kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni na kwa Moshi utafanyika Februari 26 na 27 Keys Hotel kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni.
“Usajili wote lazima ukamilike ndani ya siku hizo tatu, hakuna usajili utafanyika siku ya mashindano,” alisema.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ndio wadhamini wakuu wa mbio hizo, Pamela Kikuli, aliwataka washiriki wajisajili kwa wingi na kuyafanya mashindano ya mwaka huu yawe makubojiandikisha wa zaidi.
“Tunatarajia mashindano makubwa zaidi nay a kusisimua mwaka huu kwani kadri tunavyojisajili ndivyo unajiwekea nafasi kubwa ya kushinda mbio hizi,” alisema.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha ambaye kampuni yake inadhamini mbio za kilomita 21 nusu marathon, alisema wana imani mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa zaidi na kuwa wameandaa shughuli mbalimbaliz a kusisimua kabla na siku yam bio hizo.
Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi aliwakumbusha washiriki wote wajisajili kwa wakati na kuzingatia tarehe zilizoanishwa ili wasifungiwe nje ya usajili huku akisisitiza kuwa kampuni yake itagharamia usafiri, malazi na chakula kwa washiriki wao wote.
“Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kununua na kutumia bidhaa zetu hivi kutuwezesha kudhamini matukio kama haya,” alisema.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Oscar Shelukindo ambaye anadhamini mbio za kilomita tano maarufu kama ‘fun run’ alisema mbio hizo ziko wazi kwa watu wa umri zote hivi kuwaomba wajisajili kwa wingi na wategemee makubwa kutoka kwa kinywaji hicho.
Mbio za mwaka huu zitakazofanyika Jumapili Februari 28, Zinadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Tigo, GAPCO, Grand Malt, KK Security, Kilimanjaro Water, CMC Automobiles, FNB, TPC Limited, Kibo Palace Hotels, RwandAir na Keys Hotel.










