SportpeSa yarejea tena Kenya, KuipeleKa Hull City

25Apr 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
SportpeSa yarejea tena Kenya, KuipeleKa Hull City

KAMPUNI ya Kubashiri Ma- tokeo Michezoni ya Sport- Pesa, imeingia mkataba wa miaka minne ya kudhamini Ligi Kuu ya Kenya huku pia ikijiandaa kuipeleka nchini humo klabu ya Hull City ya England.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SportPesa, Ronald Karauri (katikati), wakati akitangaza kampuni hiyo kuingia mkataba wa kudhamini Ligi Kuu ya Kenya nchini humo juzi, ambayo sasa itajulikana kama SportPesa Premier League, pamoja na kuendelea kuidhamini klabu ya Gor Mahia FC na AFC Leopards. Kushoto ni Mwenyekiti wa AFC Leopards, Dan Mule na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo Kenya, Balozi Peter Kaberia. PICHA: SPORTPESA

Mbali na kudhamini ligi hiyo ita- kayojulikana kwa jina la ‘Sportpesa Premier League’, pia kampuni hiyo imeendelea kuwa mdhamini mkuu wa klabu za Gor Mahia FC na AFC Leopards.

Mwaka jana kampuni hiyo ili- fanikisha kuileta klabu ya Everton hapa nchini huku pia ikiendesha mashindano maalum ya ‘Sport-

Pesa Super Cup’ ambapo Gor Mahia iliibuka mabingwa na kucheza mchezo maalum na Everton katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Tunafuraha sana kuingia mka- taba mpya na washirika wenzetu wanne. Kama tulivyoendelea, kue- ndeleza vipaji vya soka kama lengo kuu kwa kampuni yetu, “alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa Kenya, Kapteni Ronald Karauri.

“Licha ya vikwazo vya sera za kiuchumi tulivyopitia kwa miezi mich- ache iliyopita, kama ilivyo ada nia yetu itabaki pale pale kwa kuunga mkono michezo ya ndani ya nchi na kuifanya Kenya kujulikana duniani kupitia mpira wa miguu”, alisema.

Hull City kutua Kenya. Akizungumza ujio wa timu kuto- ka England ambayo pia inadhamini- wa na kampuni hiyo, Karauri, alise- ma Hull City imepangwa kufanya safari ya kihistoria nchini Kenya na kwamba itakuwa alama kubwa kwa malengo ya maendeleo ya soka nchini humo.

Ziara ya timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza ‘Championship’ England, ina lengo la kuinua wachezaji wa ndani kwe- nye mashindano ya kimataifa na kuongeza nafasi yao kwenye sekta ya mpira wa miguu duniani.

Timu hiyo ikiwa Kenya itacheza mchezo maalum na moja ya klabu ya nchini humo AFC Leopards au Gor Mahia.