Mshambuliaji huyo anayewania tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika anayecheza barani, aliyasema hayo katika mazungumzo yake na Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye jijini Dar es Saaam jana.
Samatta alisema kuwa katika mazungumzo yake ya awali na klabu hiyo ya Ubelgiji, wameafikiana na atasaini mkataba wa miaka minne na nusua kama uongozi wa TP Mazembe ya DRC utamaliazana na klabu hiyo ya Ulaya.
“Tumefikia makubaliano ya awali na Genk, kilichobaki ni TP Mazembe kumalizana nao maana mimi bado nina mkataba na Mazembe (utakaomalizika Aprili mwakani),” alisema Samatta.
Aidha, Samatta aliweka wazi lengo lake la kutembelea ofisi za wizara hiyo kuwa ni kupata baraka za serikali kabla ya kwenda Nigeria kwenye sherehe za tuzo za Wanasoka Bora wa Afrika mwaka huu.
Samatta atakayeondoka nchini Januari 5 mwaka huu kwenda Nigeria, ametinga hatua ya mwisho ya nyota watatu wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza Afrika pamoja na Robert Kidiaba wa TP Mazembe na Baghdad Boundjah wa Algeria anayecheza kwenye kikosi cha Etoile Sportive du Sahel ya Tunisa.
Katika tuzo ya Mwanasoka Bora wa Jumla wa Afrika, walioingia fainali ni Andre Ayew wa Ghana na Swansea City, Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borussia Dortmund na Yaya Toure wa Ivory Coast na Manchester City, anayeshikilia tuzo hiyo.
Washindi wa tuzo hizo zitakazotolewa usiku wa Januari 7 mwakani, wapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na makocha wa vyama na mashirikisho ya soka ya nchi zote wanachama wa CAF.
Kwa upande wake, Nape amempongeza Samatta kwa mafanikio yote aliyoyapata mwaka huu, ikiwamo kuibuka Mfungaji Bora wa Klabu Bingwa Afrika, kutinga hatua fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora Afrika na kuwa mbioni kujiunga na Genk.
Samatta alijiunga na Mazembe mwaka 2012 akitokea Simba aliyoitumikia kwa msimu mmoja baada ya kujiunga nayo akitokea African Lyon (zamani Mbagala Market).
Samatta akubali miaka minne Ubelgiji
31Dec 2015
Nipashe
Samatta akubali miaka minne Ubelgiji
STRAIKA wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, amesema amefikia makubaliano na KRC Genk, lakini TP Mazembe ndiyo wanaomkwamisha kujiunga na klabu hiyo ya Ubelgiji.
Mbwana Samatta, akiwa mazoezini









