Hapo utakuta watu wanashika mabango yenye ujumbe wa namna mbalimbali, lakini kulia au kushoto, juu au chini zinaangukia ama kutetea au kusifu maslahi ya kinamama.
Ni aina ya ujumbe unaozungumzia mustakabali wa mwanamama katika mfumo na maisha yake endelevu wakati wote, katika dhana ya maendeleo endelevu.
Msingi uliko, kila ujumbe unaobebwa huwa una maana yake kubwa kwa kumtoa mwanamke sehemu moja kwenda sehemu nyingine, kutoka ngazi moja hadi nyingine.
Hivi karibuni washiriki wa semina za jinsia na maendeleo GDSD nchini, walijadili mada iliyokuwa ikisema
kuelekea Siku ya Wanawaake Duniani, maana yake imeshapita, iliangalia ni ulikosimama mtazamo wa jamii katika maendeleo endelevu ndani ya maslahi walio nayo.
Mshiriki wa mjumuiko huo wa GDSD, Jamal Juma, anasema kinachotakiwa sasa ni kutoa mfumo mzizi wa dume ambao bado upo katika maisha, ukionyesha hali ya mwanamke kutokubalika katika kushika madaraka katika baadhi ya familia.
Anasema mwanamke anapowezeshwa ana nafasi, hivyo cha muhimu kinachotakiwa ni kuwapo usawa wa kijinsia uwepo kati yake na mwanaume.
Pia ni mtazamo unaosonga kwamba hata utendaji wa jinsia, mwanamama ana uwezo wa kumiliki ardhi na hatua ilikofika ni kwamba, kinamama wanaaminiwa katika nafasi za utendaji.
Hawa Ally, anasema serikali inatakiwa iendane na kasi katika kumpatia maendeleo mwanamke, akitumia kauli
"mwanamke akiwezeshwa ana uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo katika eneo hilo."
Kuhusu maendeleo endelevu katika maeneo wanayoishi, Zuwena Shabani, anasema kuwapo kwa barabara zenye lami katika maeneo yao kumewasaidia, sasa biashara zimeongezeka, nyumba za kupanga nazo zimekuwa nyingi, hata kupangishwa watu wa aina mbalimbali, wakiwamo wasomi wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.
"Kuwapo kwa uzuri wa barabara kumesaidia nyumba kuboreshwa kuongezeka kwa biashara katika maeneo hayo na hali hiyo kumfanya mkazi wa eneo hilo kuwa na maendeleo," anasema.
Robert James, mshiriki wa GDSD anasema, kuwapo maendeleo endelevu maana yake ni kwamba, hata vizazi vinatakiwa kufikia mkanufaika na maendeleo hayo.
Anasema rasilimali zinapaswa kusimamiwa vizuri, ili ziwe na nafasi ya kuwanufaisha watu na vizazi vyao katika mtazamo huo endelevu.
Maoni yangu ni kwamba, yanayojiri katika mandhari ya kijinsia na hususan kumwendeleza mwanamke, ina maana katika tafsiri pana na ya mwanadamu na jamii inavyoishi.
Huyu wa jinsia ya kike akiwezesha na hata akasimama imara ndani ya mfumo wake kijamii, iwe kiuchumi na hata kisiasa au mengineyo ndani ya mustakabali wetu wa kimaisha, ni wazi atakuwa anasonga mbele.
Kwa asili ya binadamu, mara zote anaishi ndani ya mjumuiko wa kijamii ambao unategemeana katika namna nyingi. Hapo kijinsia ni kwamba, kuanzia kimaumbile na asili, jinsia ya kile na kiume zinategemeana, hivyo inapoleta uhalali namna upande mmoja ukautegemea upande mwingine.


.jpg?itok=nfwjwDzv)








