Hiyo inatokana na ukweli kwamba, kwa mara ya kwanza mwaka huu, wanafunzi waliochaguliwa kuingia sekondari katika shule mbalimbali za sekondari wameanza masomo kwa pamoja.
Miaka ya nyuma ilizoeleka wanafunzi kuanza masomo ya kidato cha kwanza kwa awamu, sababu kubwa ikiwa ni uhaba wa madaraka uliokuwa ukizikumba shule mbalimbali za sekondari.
Lakini, kwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya sita, zimechangia kuondoa tatizo hilo, na kilichobaki ni kuweka mikakati ya kuhakikisha uhaba wa madawati unamalizika.
Mikakati hiyo iwe ni pamoja na kushirikisha wananchi ambao kimsingi shule za umma ni zao, hivyo si vibaya wakaendelea kujitolea kuboresha miundombinu ya shule katika maeneo yao ukiwa ujenzi wa madarasa.
Kwa njia hiyo, uhaba wa madarasa unaweza kubaki historia iwapo yatajengwa ya kutosha ikiwamo kuongeza shule mpya ambao kwa namna moja au nyingine zinaweza kupunguza mrundikano wa wanafunzi madarasani.
Wakati huu wa kuelekea mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan, ni muhimu kukumbushia umma jinsi ambavyo serikali yake imejitahidi kumaliza tatizo la uhaba wa madarasa katika shule za msingi na sekondari.
Kwa mfano, ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, serikali imefanya mengi kwenye sekta ya elimu, ikiwamo kutoa Sh. bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sayansi kwa watoto wa kike, katika mikoa 10.
Serikali ametoa Shilingi bilioni 500 kuboresha elimu msingi nchini na amepokea bilioni 304 kupitia mpango wa mapambano na ustawi wa jamii dhidi ya UVIKO-19 huku bilioni 240 kati hizo zikitumika kujenga madarasa 12,000.
Hiyo ni kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (anayeshughulikia Elimu), Gerald Mweli, kwamba bilioni 60 zimejanga madarasa 3,000 kwenye vituo shikizi 907.
Katika ufafanuzi zaidi, anasema Sh. bilioni nne zimejenga mabweni 50 ya wanafunzi wenye mahitaji maalum, huku akiongeza kuwa bilioni 113 zimetolewa kujenga miundombinu ya shule za msingi na sekondari.
Anaongeza kuwa kupitia programu hizo, zimejengwa shule mpya za msingi 19 na sekondari 15 kwa gharama ya Sh. bilioni 21.25, huku fedha za tozo ya mawasiliano Sh. bilioni 7 zikitumika kukamilisha maboma ya madarasa 560.
Kwamba, maboma hayo ni ya shule za sekondari yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha elimu.
Lakini anataja Mradi wa Kuinua Ubora wa Elimu ya Sekondari Tanzania (SEQUIP), kwamba zimetolewa Sh. bilioni 130.5 kwa ajili ya kujenga shule 214 za sekondari za kata na shule 10 za wasichana za mikoa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/22.
Binafsi ninaona kuna haja ya kufurahia mafanikio hayo katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais madarakani, kuyalinda na kuyaendeleza ili kumaliza kila vikwazo vyote katika elimu.
Ikumbukwe kuwa serikali pia imeruhusu wanafunzi waliokatiza masomo wakiwamo waliopata ujauzito wakiwa shuleni, kujiuliza upya kwa kurejea masomoni ili kutimiza ndoto zao.
Hivyo, kwa uamuzi huo, ni vyema wanafunzi wenyewe watakatumia nafasi hiyo vizuri, huku wazazi na walezi pia wakiwa karibu yao kuhakikisha wanawasimamia watoto wao katika malezi ili waepuka vishawishi.
Rais ameonekana kujipambanua wazi jinsi anavyotamani kila mtoto wa Kitanzania anatimiza ndoto yake katika elimu kwa kuwekeza katika elimu ikiwa ni pamoja na mkakati wa kujenga shule za wasichana katika mikoa 10.



.jpg?itok=nfwjwDzv)







