Katika maeneo tofauti nchini hususan katika majiji yakiwamo ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Tanga baadhi ya nyumba au majumba ujenzi wake katika miaka ya karibuni hauzingatii umuhimu wa kuchimba mashimo ya kuhifadhia maji taka.
Maji taka yanayotoka kwenye vyoo, bafu na mengineyo baada ya vyombo kuoshwa au nguo kufulia yasipohifadhiwa kwa uangalifu ni kero kubwa kwa watu na makazi yao kwa ujumla.
Miaka ya nyuma, ujenzi wa nyumba za makazi ulizingatia zaidi kuwapo mashimo hayo kutokana na umuhimu wake.Lakini baadhi ya wajenzi wa nyumba wa miaka ya karibuni wanakwepa gharama za ujenzi huo.
Mazingira hayo yanasababisha maji taka kumwagwa ovyo barabarani hata kuwa moja ya vyanzo vya kuenea kwa magonjwa ya mlipuko ikiwamo kipindupindu.
Maji taka hayo hayasababishi magonjwa tu ni pamoja na athari mbaya kwa mazingira kwa sababu ya kuwa na mchanganyiko wa vitui mbalimbali ikiwamo sabuni na uchafu mwingineo.
Maji taka hayatoki katika makazi pekee bali hata katika maeneo yanayofanyiwa biashara ndogondogo ikiwamo saluni za wanawake, mama lishe, wauza matunda na kwingineko.
Wafanyabiashara hao majitaka huyamwaga mbele ya biashara zao na kusababisha hali isiyopendeza hata kidogo.
Kimsingi miongoni mwa hatua zinazostahili kuchukuliwa ni kuanza na wajenzi wa nyumba ambao hawazingatii kujenga mashimo ya kuhifadhia majitaka.
Wakaguzi wa nyumba kabla na baada ya kukamilika wahakikishe hilo wanazingatia kila mjenzi anapojenga nyumba yako afahamu kuwa ni lazima yawepo mashimo hayo.
Pamoja na kwamba, wapo wanaojenga nyumba kwenye viwanja vyenye ukubwa mdogo, basi mamlaka husika zihakikishe zinaweka ama kujenga mfumo wa maji taka utakaowalazimu wanaohudumiwa na mfumo huo kuulipia kila baada ya muda fulani.
Kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli iendane na mabadiliko ya ujenzi unaozingatia vigezo, isije kuwa tunatumia gharama kubwa kutibu na kuepuka magonjwa ya mlipukoa wakati hili tulifumbia macho.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na idara zake izingatie hili kwa kuhakikisha makazi haysongezeki kujengwa tu kila uchao bali yawe makazi bora yanayoendana na hali ya ongezeko la watu hasa mijini.
Makazi bora yakiwa na miundombinu wezeshi tutaepuka athari mbaya ikiwamo magonjwa ya mlipuko.
Makazi bora yenye mashimo ya kuhifadhia maji taka yanawezekana. Kinachotakiwa ni wajenzi waandae bajeti ya kutosha kabla ya kujenga nyumba ili kuhakikisha tunakuwa miji na majiji salama kiafya.
Makazi bora yawe na mfumo wa majitaka
05Feb 2016
Christina Mwakangale
Nipashe
Muungwana Lazima Nilonge
Makazi bora yawe na mfumo wa majitaka
MAKAZI bora ni yale yanayojitosheleza katika miundombinu hata kuwezesha kila aina ya taka inayozalishwa kuhifadhiwa ama kutupwa katika sehemu maalum kwa ajili hiyo.


.jpg?itok=nfwjwDzv)








