Azam FC, mabingwa wapya wa Afrika Mashariki na Kati, waliyaanza mashindano hayo kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya mabingwa wa Zambia, Zesco United Jumatano.
Ilikuwa sare ya pili mfululizo kwa timu hizo mbili kwani mwaka jana walitoka 2-2 katika mechi yao ya michuano maalum ya timu nne iliyofanyika DRC.
Kocha wa Azam, Stewart Hall, anaitumia michuano hiyo kurekebisha makosa ya kikosi chake kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka huu.
Licha ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi ya Bara bila kupoteza mechi hata moja, safu ya ulinzi ya Wanalambalamba inayoongozwa na Muivory Coast Serfe Wawa, imeonekana kuyumba ikiruhusu mabao 10 katika mechi 13 zilizopita za ligi hiyo msimu huu.
Mabeki Said Morad na Racine Diouf wanaonekana kushindwa kuziba pengo la Aggrey Morris ambaye yuko nje ya uwanja kwa muda mrefu sasa kutokana na majeraha ya goti.
Timu hiyo yenye taji moja la ligi ya Bara, itakamilisha ziara yake Zambia kwa kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Zanaco FC ya nchini humo Jumatano.
Azam kibaruani tena Zambia leo
30Jan 2016
Sanula Athanas
Nipashe
Azam kibaruani tena Zambia leo
- Kipre Tchetche alikuwa shujaa wa Azam aliposawazisha dakika ya mwisho goli la Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Kenya msimu uliopita, Jesse Were.
BAADA ya kuambulia sare katika mechi ya kwanza, Azam FC watakuwa na nafasi nyingine ya kupima kikosi chao kimataifa watakapowakabili mabingwa Zimbabwe, Chicken Inn katika mashindano maalum ya timu nne yanayofanyika kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia.
Azam FC









