Zari aondoka kwenye nyumba ya Diamond Afrika Kusini

25Oct 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Zari aondoka kwenye nyumba ya Diamond Afrika Kusini

Baada ya maneno ya muda mrefu katika mitandao ya kijamii, hatimaye mwanamama Zarinah Hassan, maarufu Zari The Bosslady, ameamua kuondoka katika nyumba ya mzazi mwezake mwanamuziki Diamond Platnumz, baada ya kuwepo vitisho kuwa nyumba hiyo itauzwa akiwamo ndani pamoja na watoto wake.

Zari amefanya maamuzi ya kutoka katika mjengo huo wa Diamond uliopo jijini Pretoria, Afrika Kusini na kwenda katika nyumba yake mpya yenye muonekano wa kisasa zaidi aliyojizawadia katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa alipokuwa akitimiza miaka 39. Hiyo ni kwa mujibu wa tovuti ya Uganda online.net.

Baada ya Diamond kutengana na mwana mama huyo mwenye ushawishi Afrika Mashariki, lakini alimuacha aendelee kuishi katika nyumba hiyo pamoja na watoto wake pamoja na watatu aliozaa na marehemu Ivan.

Ikumbukwe kuwa miaka kadhaa iliyopita Diamond alimnunulia nyumba Zari kama zawadi ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa alipotimiza miaka 36 na wawili hao walikuwa wakiishi pamoja Tanzania na Afrika Kusini.