Akizungumza na Lete RAHA, Mzozo alisema wamejipanga kuwashangaza wapenzi wa soka wa jiji la Dar es Salaam kwa kuing'oa Yanga kwenye michuano hiyo inayotoa mwakilishi wa nchi katika Kombe la Shirikisho Afrika.
“Yanga ni klabu kubwa na ina wachezaji wazuri, lakini hatuwaogopi kwa kwakuwa na sisi tuna wachezaji vijana ambao wanajituma na tunaamini wanaweza kufanya makubwa wanapokuwa uwanjani. Tofauti yetu na Yanga ni kuwa hao wanacheza Ligi Kuu na sisi Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
“Watu wasifikiri timu za FDL ni timu ndogo, tena wasidhani kama zitashindwa na timu kubwa kama Yanga. Timu za kwenye ligi yetu ndizo zinazoongoza kwa kutoa wachezaji wakubwa. Wachezaji wa huku wanacheza kwa kujituma sana kwa ajili ya kujiuza.
“Pia sisi tunacheza mechi nyingi za ligi kwa muda mfupi ukilinganisha na timu za Ligi Kuu hivyo tuna uzoefu wa kupambana kwenye mazingira magumu kwa muda mfupi,” alisema.
Timu ya Friends Rangers kwa vipindi tofauti imekuwa ikitoa wachezaji ambao wametamba katika Ligi Kuu Tanzania bara kama Haruna Moshi 'Boban', Jabir Azizi, Athuman Machupa, Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ na wengine wengi.
Friends Rangers yaikamia Yanga balaa
20Jan 2016
Lete Raha
Friends Rangers yaikamia Yanga balaa
MABINGWA wa Tanzania Bara, timu ya Yanga imepigwa mkwara mzito na Mkurugenzi wa Ufundi wa Friends Rangers, Heri Mzozo, kuelekea mechi yao inayokaribia ya Kombe la Shirikisho (FA).










