Alhamisi iliyopita, Simba iliichapa Ndanda FC mabao 3-0, Kiiza alifunga magoli mawili na kufikisha idadi hiyo na kumzidi Amiss Tambwe wa Yanga mwenye magoli 17.
Kwa idadi hiyo ya magoli, ina maana yeyote atakayekuwa mfungaji bora msimu huu, atavuka idadi ya kuwa amefunga magoli mengi zaidi kuliko yaliyofungwa na Msuva msimu uliopita. Hadi sasa Msuva ana mabao sita tu.
Hata hivyo, Kiiza, Tambwe na Donald Ngoma wa Yanga ndiyo wanaoonekana kuwa vinara wa kupachika mabao. Ngoma ana magoli 13.
Kama washambuliaji hao watasinzia, basi Jeremiah Juma wa Prisons mwenye magoli 11, Elius Maguri wa Stand United magoli 10, Kipre Tchetche wa Azam na Ibrahim Ajibu wa Simba wenye magoli tisa wanaweza kuwaweka kwenye hali ngumu.
Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Abdallah Juma anashikiria rekodi ya kufunga mabao mengi aliyoiweka mwaka 2006 alipofikisha mabao 24 na bado kuvunjwa hadi sasa.










