-Jwaneng Galaxy ya Botswana Jumamosi katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, iliyopewa jina la 'Vita ya Kisasi.'
Mechi itakayochezwa leo, awali ilipigwa kalenda kutokana na Simba kusafiri kwenda nchini Ivory Coast kukabiliana na Asec Mimosas katika mechi ya raundi ya tano ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Felix Houphouet Boigny jijini Abdijan Ijumaa iliyopita na kumalizika kwa suluhu.
Mchezo huo utakamilisha mechi ya 16 kati ya timu 32 zilizotakiwa kucheza hatua hiyo ya raundi ya tatu ya kombe hilo ili kusaka bingwa atakayeiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao.
Tayari jumla ya mechi 15 zimeshachezwa na mechi ya leo itakamilisha idadi ya michezo 16, kabla ya kupangwa kwa ratiba nyingine kwa ajili ya michezo ya kwenda robo fainali.
Kocha Mkuu wa Simba, Benchikha, amesema mechi ya leo ina umuhimu kwake mara mbili kwa sababu inamwezesha kuchezesha wachezaji wengi ambao atawatazama na kuangalia kama wanaweza kumpa kitu Jumamosi katika mechi muhimu ya Ligi ya Mabingwa, lakini kuangalia kile ambacho amekifundisha na kukirekebisha uwanja wa mazoezi baada ya mechi iliyopita.
"Kulikuwa na mapungufu kadhaa katika mechi iliyopita hasa ya kutumia nafasi, tumelifanyia kazi mazoezini, nataka niangalia leo kama limepungua kwa kiasi gani, hiyo ni moja, lakini nitawatumia baadhi ya wachezaji ili niwaangalie kama wanaweza kunipa angalau kitu katika mechi ya Jumamosi na pamoja na yote tunahitaji kushinda mechi hii ili tuwe kwenye njia ya kuchukua Kombe la FA, pamoja na kuwafurahisha mashabiki wetu," amesema Banchikha.
Wakati huo huo, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally, amesema mchezo wa Jumamosi si tu kwamba utakuwa ni wa kusaka ushindi ili kwenda hatua ya robo fainali, bali ni wa kulipiza kisasi cha kufungwa na timu hiyo, Oktoba 24, 2021 kwenye Uwanja wa Banjamin Mkapa.
"Sidhani kama kuna Mwanasimba amesahau machungu ambayo tumewahi kuyapitia na niwaibie siri, Rais wa Heshima wa Klabu, Mohamed 'Mo' Dewji, aliugua wiki mbili kutokana na maumivu tuliyoyapata ambayo tulisababishiwa na Jwaneng Galaxy, nadhani sasa muda umefika wa kwenda kufuta haya maumivu. Tunakwenda kulipa kisasi, ni muda wetu sasa na mchezo huu tumeupa jina la 'Vita ya Kisasi'," amesema Ahmed.
Amesema katika mechi hiyo wanahitaji vitu viwili, kutinga robo fainali na kulipa kisasi kitu ambacho kimewafanya kwa sasa kuwa kwenye maandalizi makali kwa ajili ya mchezo huo.
Simba ilichapwa mabao 3-1 kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kushindwa kuingia makundi kwa tofauti ya mabao ya nyumbani na ugenini baada ya matokeo ya jumla kuwa 3-3.
Na hii ni baada ya Simba kushinda mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ugenini, Oktoba 17, 2021, Jwaneng Galaxy ikasonga mbele kwa kufunga mabao mengi ugenini, Wekundu wa Msimbazi wakashindwa kutinga makundi na kwenda Kombe la Shirikisho ambalo huko walifikia hatua ya robo fainali.