Kampuni hiyo ndio mdhamini mkuu wa mbio hizo za halfa marathon ambapo wamehakikisha huduma zote muhimu zinapatikana siku ya mbio hizo.
Akizungumzia mbio hizo, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo, amesema kampuni hiyo imejipanga kuwahudumia wanariadha na wateja wa tigo watakaofika kwenye mbio hizo za Kimataifa.
"Tumejipanga kutoa huduma nzuri, kutakuwa na Wi-Fi Spots ya 4G ya bure kwa watu wote watakaofika kwenye viwanja vya Ushirika na maeneo mbalimbali ya Moshi mjini hasa Moshi Club ambapo tamasha la Kili Marathon litafanyika," amesema Kinabo.
Amesema kiujumla maandalizi yote ya mbio hizo za yamekamilika na wanategemea wageni wataanza kumiminika mkoani humo kuanzia leo.
Kampuni ya Tigo inayoongoza kwenye mapinduzi ya kidigitali hapa nchini kwa mara nyingine imeendelea kudhamini mbio hiozo za half marathon ambapo kwa mwaka huu zitafanyika Jumapili ijayo.










