Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme wakati akizungumza na watumishi wa idara ya afya kutoka Halmashauri za Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama kama sehemu ya kuwakumbusha wajibu wao na kuagiza wale wanaobainika kwenda kinyume na misingi ya kazi zao wawajibishwe kisheria nasio vinginevyo.
Amesema, hivi karibuni pia kuna watumishi wa hospitali hiyo walisimamishwa kazi kwa utovu wa nidhamu iliyosababisha kifo cha mjamzito aliyefika kujifungua na kukosa huduma ya kujifungua, watumisi hao ni Christina Kulwa Dk. Daraja la II, Joyce Shidayi Ofisa Mteknolojia msaidizi daraja la kwanza, Silya Kuchibanda Ofisa Muuguzi Msaidizi daraja la kwanza, Betina Lwamuziga Ofisa Muuguzi Msaidizi daraja la kwanza, Nuru Philipo Ofisa muuguzi daraja la pili na Lemi Majige Muuguzi daraja la kwanza.
Aidha, Mndeme amesema misingi ya kazi ya sekta ya afya haielezi kuwatolea mimba watu na badala yake mnayatenda haya na kuhatarisha usalama wa wanafunzi, hivyo siwezi kuingilia Mahakama ila najua watatoa hukumu kulingana na ushahidi watakaoupata.
Amesema, serikali imekuwa ikitengeneza mazingira mazuri ya kutolea huduma lakini wachache wasiokuwa na maadili ya kazi wanaichafua sekta hiyo kwa kufanya vitu vya hovyo, na kumwagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuwaondoa kwenye nafasi zao Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo na Mganga Mfawidhi kwa kushindwa kusimamia vema majumu yao hadi haya yanatokea.










