Wakati nipo Brazil nilikuwa nakikumbuka sana chama changu kipindi cha siku za mapumziko nilikuwa navaa shati langu la kijani na suruali nyeusi, msaidizi wangu akaniambia hakuna weekend kwenye ofisi za Serikali," amesema Dk Nchimbi.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM waliofika kumpokea alipowasili kwenye shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha kwa ajili ya kikao na Makatibu kutoka vyama sita vya Ukombozi Kusini mwa Afrika.
Alisema laiti angefahamu kuwepo kwa wanachama wa chama hicho kuja kumpokea angevaa sare za chama afanane nao wapendeze pamoja.
Kuhusiana na uchaguzi Dk.Nchimbi ametaka wanachama kuchagua viongozi wenye maadili wanaowaheshimu watu.
Katibu huyo anaungana na Makatibu wakuu kutoka vyama sita vilivyoshiriki harakati za Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika ambavyo ni ANC (Afrika kusini), SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), MPLA (Angola), ZANU PF (Zimbabwe) na CPC Chama Cha kikomunisti cha nchini China.










