Wachezaji 6 wanaostahili kuuzwa Manchester Utd

24Jul 2023
Na Mwandishi Wetu
UINGFEREZA
Nipashe
Wachezaji 6 wanaostahili kuuzwa Manchester Utd

WAKATI dirisha la usajili la majira ya joto likizidi kupamba moto, Manchester United inajikuta katika njia panda kwenye harakati zake za kuwafikia wenye nguvu. Ili kuimarisha kikosi, 'Mashetani Wekundu' hawana budi kuzingatia si tu kupata vipaji vipya bali pia kuwaondoa baadhi ya wachezaji.

 

Mengi yamesemwa kuhusu wanaotarajiwa kusajiliwa na Manchester United katika msimu huu wa majira ya joto. Katika makala haya, tunawaangalia wachezaji sita ambao 'Mashetani Wekundu' hao wanatakiwa kuwauza ili kurahisisha orodha yao mpya...

 

#6. Anthony Martial

Baada ya kuwa na wakati mgumu alipotolewa kwa mkopo kule Sevilla, Anthony Martial, ameendelea kukatisha tamaa kwa Manchester United. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa anaendelea kuwa pasua kichwa kwa kocha Erik ten Hag na anaongoza orodha hii ya wanaohitajika kuuzwa.

Kiwango cha Mfaransa huyo wakati alipokuwa Old Trafford kimekuwa si cha kuridhishwa na sasa unaweza kuwa wakati wa kuanza upya. Kumuuza Martial si tu kutaiingizia fedha nyingi, bali pia malipo yake makubwa ya mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki ni sawa na matumizi yasiyo na tija.

 

#5. Fred

Fred amekuwa na wakati mgumu kupata uthabiti wowote katika Klabu ya Manchester United tangu aliposajiliwa hapo mwaka 2018. Usajili wa hivi karibuni wa Mason Mount unamaanisha kuwa atakuwa na muda mchache wa kucheza na kuongeza ushindani kwenye safu ya kiungo, na hivyo kudumaza maendeleo ya Mbrazil huyo.

Huku akiwa amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa katika klabu hiyo, itakuwa ni kwa manufaa kwa mchezaji na klabu kuachana. Ofa ya Galatasaray ilikataliwa na Manchester United kwa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Brazil kama ilivyoripotiwa na Fabrizio Romano na amekuwa pia akiwaniwa na klabu za Saudi Arabia na Fulham.

 

#4. Jadon Sancho

Jadon Sancho amekuwa duni tangu arejee England, na hivyo kuzuia kiwango cha juu kilichotarajiwa kutoka kwa mchezaji huyo cha pauni milioni 75. Ingawa fowadi huyo ameonesha machache juu ya uwezo wake siku za nyuma, muda wake Manchester United kwa ujumla umekuwa wa kukatisha tamaa. Idadi yake ya mabao 12 katika mechi 79 alizocheza kwenye ligi hiyo ni mbaya kutokana na mchezaji anayelipwa mshahara wa pauni 350,000 kwa wiki.

Sancho amekuwa akihusishwa na kurejea Borussia Dortmund, huku Tottenham Hotspur na Brighton & Hove Albion zikimwania katika kipindi hiki cha majira ya joto. Raia huyo wa England ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi zaidi pale Old Trafford huku akiwa hana kiwango cha kuvutia. Manchester United itafanya vema kama itaamua kumuuza.

 

#3. Brandon Williams

Brandon Williams alipoingia uwanjani alionekana kama tegemeo la kusisimua, akionesha uwezo wake mwingi kama beki wa pembeni na winga. Hata hivyo, ujio wa Erik ten Hag umemfanya kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Williams ameona muda wake wa kucheza ukipungua kwa kiasi kikubwa na hakuna dalili za kuona kama muda utaongezeka. Uhamisho wa kudumu kwa klabu ambapo anaweza kupata dakika za kawaida itakuwa na manufaa kwa maendeleo yake. Beki huyo wa England anazidi kuonekana kutoshiriki katika mipango ya Man United.

 

#2. Harry Maguire

Maisha ya Harry Maguire katika Klabu ya Manchester United yametatizwa tangu alipowasili kutoka Leicester City kwa mkataba wa rekodi ya dunia wa pauni milioni 80, mwaka 2019. Ingawa nyota huyo wa kimataifa wa England ana kipaji kisichopingika, amekuwa na ugumu kuingia kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Erik ten Hag.

Kwa uwapo wa Lisandro Martinez na Raphael Varane wanaopendelewa zaidi na kocha, itakuwa bora kwa Maguire kuhama. 'Mashetani Wekundu' hao wameripotiwa kutaka kumpiga bei kiasi cha pauni milioni 50, huku klabu ya Tottenham Hotspur ikijatwa kumuwania.

 

#1. Donny van de Beek

Donny van de Beek aliwasili Manchester United akiwa na matarajio makubwa kutoka Ajax ambako alikuwa chini ya kocha wa sasa Erik ten Hag. Hata hivyo, kiungo huyo wa kati wa Uholanzi amekuwa na wakati mgumu kufanya mabadiliko na amejitahidi kupata utimamu wa mwili au kujiamini.

Inaweza kuwa manufaa kwa pande zote mbili kuachana na kumruhusu Van de Beek kwenda kutafuta malisho sehemu nyingine.