-hivi karibuni na kuanza shughuli zake baada ya kukamilika kwa asilimia 100.
Hatua hiyo imekuja kufuatia wiki ya mazingira sambamba na kituo hicho kuwa mbioni kuzinduliwa lengo likiwa ni kuhimiza utunzaji wa mazingira katika kituo hicho kitakacho hudumia watu kutoka mikoa mbalimbali ndani ya Tanzania na nje nchi.
Akizungumza wakati wa zoezi shughuli hiyo, Balozi Mabanzo amesema kuwa, jitihada zinafanyika kwa kiwango kikubwa kuwapa elimu wananchi juu ya utunzaji wa mazingira kutokana na mazingira kuwa msaada mkubwa kwa viumbe vyote vinavyoyazunguka.
“Tutahakikisha maeneo ya standi sambamba na yale yanayoizunguka stendi hii yanakuwa safi na salama ili kuwezesha wananchi na watumiaji wa stendi hii kuwa sehemu salama na tutaweka mabango yanayoonyesha utunzaji wa mazingira na kutakuwa na sehemu za kutupa taka katika maeneo haya,” amesema.
Naye, Mwenyekiti wa stendi kuu ya mabasi Nyegezi, Noel Lucas Mbise, amesema kuwa elimu itatolewa kwa madereva na watumiaji wa stendi kuu ya Mabasi Nyegezi ili kuunga jitihada za udhibiti wa uchafuzi katika eneo hilo.
“Elimu ni Muhimu kwani siku zote kuna msemo usemao kitunze kidumu, hivyo basi hata stendi yetu ya mabasi tukiitunza kwa kuweka mazingira safi na salama itapendeza zaidi na kuwa sehemu yenye mvuto pia kwani uwepo wa miundombinu ya kisasa unahitaji uangalizi mkubwa na elimu kwa watumiaji,” ameeleza.
Kwa upande wake, Erick Alphonce ambaye ni Wakala wa Mabasi, ameeleza kuwa tatizo kubwa lililopo katika stendi hiyo linasababishwa na wauzaji wa miwa kutokana na kiwango kikubwa cha taka kutokanana na Maganda, hivyo amewaomba wafanyabiashara hao kutunza mazingira.
Anastazia Michael ni kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo cha Kaliua amesema kuwa wamechagua stendi hiyo kuwa sehemu ya kufanyia usafi kwa siku hiyo kwani inaenda kuanza kutumika kwa wahitaji hivi karibuni.










