-hivyo kwa sasa inapiga mazoezi mara mbili kwa siku ikianzia gym hadi uwanjani.
Jana asubuhi Yanga ilifanya mazoezi ya gym Gymkhana, Dar es Salaam kwa saa mbili na jioni walifanya ya uwanjani katika kambi yao ya Avic Town, Kigamboni kwa saa mbili chini ya Kocha wa Viungo, Helma Gueldich.
Mazoezi hayo yameelezwa ni kwa ajili ya kutafuta stamina na yalihudhuriwa na wachezaji wote huku kiungo Bernard Morrison aliyekuwa majeruhi akiwa sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, alisema anafahamu vizuri mbinu za US Monastir na wanavyocheza, hivyo wamelazimika kuongeza muda wa mazoezi ikiwamo kwenda gym kutafuta stamina.
Alisema mechi itakuwa ya ushindani mkubwa kwa sababu wanahitaji kusaka ushindi wa alama tatu ili kufanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
“Tutakuwa na mazoezi ya aina mbili, asubuhi tunafanya gym na jioni uwanjani, hii mechi ni ngumu sana maana tumeona jinsi tulivyocheza mechi ya kwanza, mapungufu yaliyojitokeza tunayafanyia kazi kuelekea mechi yetu ijayo.
"Kuna wachezaji wanakosa mwendelezo, leo wanacheza vizuri mechi inayofuata wanaonesha kiwango cha chini hilo sifurahishwi nalo, kitu ambacho kwa sasa nakifanyia kazi,” alisema Nabi.










