Mremi asema Simba chanzo kushinda mil. 11/- SportPesa

15Mar 2023
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mremi asema Simba chanzo kushinda mil. 11/- SportPesa

MKAZI wa Tabata Liwiti, Charles Ndechihiko Mremi, amejishindia kitita cha Sh. 11,555,580, ikiwa ni Bonus ya Jackpot ya SportPesa baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 alizocheza.

Mshindi wa Jackpot Bonus, Charles Mremi kutoka Tabata, Dar es Salaam, akionyesha mfano wa hundi ya Sh. milioni 11.5 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13.

Akizungumza katika Ofisi za SportPesa Oysterbay, Dar es Salaam jana, Mremi alisema alianza kucheza na SportPesa kuanzia mwaka 2020, baada ya kuona jina la kampuni hiyo katika jezi za Simba ambayo ni shabiki mkubwa wa timu hiyo.

"Mimi nilianza kucheza SportPesa mwaka 2020, nilikuwa nanunua jezi kila zilivyokuwa zinatoka kila msimu. Kwa miaka ile Simba ilikuwa vizuri sana na kila nilipokuwa nikinunua jezi nilikuwa nakutana na jina la SportPesa.

"Nilipofuatilia niligundua kumbe hii ni kampuni ya kubashiri na kujua kwa undani wanafanyaje fanyaje kwenye biashara yao," alisema.

Charles anaendelea kusema wakati ameanza kucheza miaka miwili iliyopita alikuwa anashinda Sh. 11,000, laki mbili, laki tatu na nyingine ndogo ndogo, ambazo zilimpa moyo wa kendelea kubashiri kila alipopata nafasi.

Kuhusu mkeka huo wa Jackpot alioshinda, Mremi alisema aliziona mechi za Jackpot Jumatatu iliyopita na kuweka mkeka wake siku hiyo hiyo, baada ya kupitia kwa kuangalia historia ya timu, magoli waliyofunga na pointi walizonazo katika msimamo wa ligi.

‘’Naweza kusema Mungu ni mwema sana kwangu, kwani kwanza, nilishinda mkeka wakati nikiwa ninaumwa na nimetoka hospitali. Charles anasema yeye ana kawaida ya kila Jumatatu na Alhamisi au Ijumaa kuweka mikeka ya Jackpot za SportPesa.

Mimi nina kawaida ya kuweka japo 2000 au 3000 kwenye simu yangu na kisha kucheza Jackpot za SportPesa ambazo moja huchezwa katikati ya wiki na nyingine mwishoni mwa wiki.

"Katika mkeka wangu huu ulioshinda nilicheza majira ya saa sita mchana. Kawaida huwa sina muda wa kufuatilia matokeo ya mechi nilizocheza, mpaka zikiisha ndio nasubiri kuona sms kama nimeshinda au la. Sasa kwa mkeka huu ilikuja sms ya hongera lakini kwa muda ambao sms inaingia nilikuwa sebuleni kwangu nimepumzika naangalia muvi, baada ya kutoka hospitali.

"Sikutumia simu yangu kwa muda, lakini sms ya hongera ilikuwa tayari imeshaingia. Baadaye kidogo nilipigiwa simu na mtoa huduma nikiulizwa kama nimeona sms. Kwa kuwa nilikuwa ninaumwa sikutilia maanani na nikajibu sijaona sms wanayoniambia, baada ya muda kidogo nilijaribisha kuwasiliana na namba iliyonipigia kwa kufanya kama natuma Tigo Pesa. Zoezi hilo halikufanikiwa hivyo ikanipa hisia labda ni matapeli wanajaribu kunichezea akili wanipige hela," alisema na kuongeza.

"Nilikumbuka kwamba nina jamaa yangu Juma Pembe.

Juma anashiriki sana kwenye kubeti. nilimwelezea kilichojiri na yeye akashauri tutafute kwenye mtandao (google) ofisi za SportPesa zilipo kisha tundwe, ilipotimu asubuhi, Juma alinitumia ramani na nikaifuatisha mpaka kufika. Kwa kweli nimefurahi sana kwa kuwa tangu nimefika nimepokelewa vizuri na kupitishwa katika hatua mbali mbali za uhakiki za kiofisi na sasa nimetoka kukabidhiwa hundi ya pesa niliyoshinda.’

Akizungumzia fedha hizo ataifanyia nini, alisema kitu cha kwanza atafanya ni kufungua na kuwawekea kiasi cha fedha watoto wake wawili ambao bado ni wadogo sana.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya SportPesa, Sabrina Msuya, alimpongeza Mremi kwa ushindi wake na kumtaka aendelee kucheza kwani bado Jackpot kila wiki inazidi kuongezeka.