Aidha, bodi ya wadhamini wa klabu hiyo, imeuagiza uongozi kuitisha mkutano kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Juni 5 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Francis Kifukwe aliyeongozana na Fatuma Karume na Jabir Katundu alisema TFF ina jukumu la kuagiza kufanyika kwa uchaguzi, lakini haina mamlaka ya kusimamia.
Kifukwe alisema wanasubiri kumalizika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la FA ndipo waanze mchakato wa uchaguzi.
Akizungumzia kuhusiana na kadi zitakazotumika, Kifukwe alisema hatima itajulikana kabla ya uchaguzi.
"Kuhusu mambo ya katiba na kadi zitakazotumika, mambo yote yatajulikana kabla ya uchaguzi," alisema Kifukwe.
Naye Fatuma Karume alisema wao kama wadhamini wa bodi hiyo wanajipanga kuhakikisha uchaguzi unakwenda kama ulivyopangwa .
"Sisi tuko imara, tunasubiri tumalize Ligi, FA na mechi dhidi ya Angola kisha tuanze maandalizi ya uchaguzi," alisema Karume.










