Sare hiyo ni furaha kubwa kwa Yanga, ambayo sasa bila shaka itakuwa imeshusha presha baada ya Azam kubanwa na kutoa nchi ya kunyakua taji.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Simba ilishindwa kabisa kumaliza kiu ya mashabiki wake, waliondoka wakiwa wameinamisha vichwa chini.
Kabla ya mchezo huo, Simba walikwenda Zanzibar kupiga kambi ya wiki nzima ili kuhakikisha inapata ushindi kwenye mechi hiyo waliyoambulia pointi moja na kufikisha 58, huku Azam wakiongeza pointi moja na kufikisha 59 na kubaki nafasi ya pili nyuma ya Yanga inayoongoza baada ya kukusanya pointi 65.
Katika mechi hiyo, timu zote zilikosa nafasi kadhaa za kufunga, huku Azam ndiyo wakionekana kushindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga.
Kocha Msaidizi wa Simba, Adam Abdallah alisema pamoja na sare hiyo bado hawajakata tamaa katika mbio za kusaka ubingwa.










