Wateja wa betPawa wajishindia sh.bilioni 53.8 ndani ya siku 10

02Nov 2023
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Wateja wa betPawa wajishindia sh.bilioni 53.8 ndani ya siku 10

Umekuwa ushindi uliovunja rekodi kwa wateja wa betPawa nchini Tanzania, ambao walijishindia sh.bilioni 53.8 ndani ya siku 10.Wateja 335,706 tofauti walisherehekea ushindi wakati wa mafanikio ya kuweza kubashiri kwa usahihi kwenye michezo kati ya Jumamosi Oktoba 21 na Jumatatu Oktoba 30 mwaka huu.

Mshindi Mkubwa kuliko wote alijishindia sh.milioni 372.9  kwa dau la shilingi elfu mbili mia mbili (2,200), ikiongezewa na Bonasi ya Ushindi ya asilimia 645 kwenye mechi 50 alizobashiri.

Hii imedhihirisha kauli mbiu ya betPawa pesa kidogo, ushindi Mkubwa  (Bet Small,Win BIG) Kwa jumla wateja 3,738 wa betPawa Tanzania walibadilishwa kuwa mamilionea kwa kipindi cha ndani ya siku 10.

Kutokana na idadi hiyo kubwa ya washindi ambayo haijawahi kutokea ilisababisha ucheleweshaji wa malipo katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri.

Kwetu betPawa kuwa na washindi wengi kumesababisha akaunti zetu za mitandao ya simu kulazimika kuongezwa kiwango cha pesa kila mara kulingana na kiwango cha juu kinachoruhusiwa kwa siku.

Hata hivyo wanafanya kazi saa 24 ili kumalizia malipo ya washindi wachache waliosalia.

Meneja wa betPawa nchini, Borah Ndanyungu alisema: “Hakuna mtu bora kuliko wateja wa betPawa ambao wameweza kufanikiwa kupata ushindi MKUBWA, na katika kipindi hiki cha siku 10 wameweza kushinda zaidi kuliko hapo awali.”

Aliongeza: “Tunafahamu idadi kubwa ya ushindi umesababisha ucheleweshaji katika tasnia nzima ya michezo ya kubashiri na sisi betPawa tunafurahi kuwa tayari tumeweza kulipa washindi wengi tayari mpaka sasa. Tunafanya kazi bila kuchoka ili washindi wachache waliobakia mwisho walipwe.”