Wachezaji wa Nyumbu Fc watakiwa kupambana kupanda ligi

04Feb 2024
Julieth Mkireri
Kibaha
Nipashe Jumapili
Wachezaji wa Nyumbu Fc watakiwa kupambana kupanda ligi

WACHEZAJI wa timu ya Nyumbu FC ya Mkoani Pwani inayoshiriki michuano ya Ligi Daraja la kwanza wametakiwa kuhakikisha wanacheza kwa kujituma wakati wote ili timu hiyo iweze kupanda ligi ya Championship Msimu ujao.

Msemaji wa Nyumbu FC Mariam Songoro.

Hayo yamesemwa  na Kaimu Mkuu wa kikosi cha Jeshi la Wananchi Kambi ya Nyumbu Kanal Charles Kalambo wakati akizungumza na wachezaji wa timu hiyo waliotambulishwa kwa wadau katika hafla ya siku ya  Nyumbu iliyofanyika katika viwanja vya Nyumbu.

Kanal Kalambo pia amesisitiza nidhamu kwa wachezaji sambamba na kujitoa kwa ajili ya timu hiyo Ili iweze kufanya vizuri.

Mwenyekiti wa timu hiyo Jafar Kilindo anasema wamejipanga vizuri kuelekea mzunguko wa pili na anaamini watafanya vizuri.

Msemaji wa Nyumbu FC Mariam Songoro alisema siku hiyo ya Nyumbu iliambatana na kutambulisha jezi  na kufanya harambee ambapo ahadi na fedha taslimu zaidi ya sh. Miln Tano zilipatikana.

Mariam amesema timu hiyo inakwenda kufanya vizuri zaidi katika mechi zijazo kutokana na maandalizi yaliyofanyika huku akiomba wadau kuendelea kuiunga mkono kwa kujitokeza kuishangilia pindi inapocheza.

Katika hafla hiyo  michezo tofauti ilifanyika , ikiwa ni pamoja na kuvita kamba , kukimbiza kuku na mchezo mpira wa miguu  ambapo , nyumbu veteran  waliibuka kidedea dhidi ya Kibaha veterani.