Simba yaipiga hesabu Coastal Union

09Apr 2016
Faustine Feliciane
Dar
Nipashe
Simba yaipiga hesabu Coastal Union

SIMBA inajiandaa kucheza na Coastal Union keshokutwa Jumatatu, Aprili 11 kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Coastal Union, huku kocha Jackson Mayanja akitabiri mchezo huo kuwa mgumu kwao.

kocha wa Simba Jackson Mayanja.

Mayanja alisema kuwa ugumu wa mchezo huo unatokana na hali ya sasa ya wapinzani wao Coastal Union walio kwenye wakati mgumu kushuka daraja.

"Mchezo hautakuwa rahisi...tumecheza nao siku chache zilizopita katika mechi ya Ligi Kuu Bara na kushinda, hata hivyo haikuwa kazi rahisi," alisema Mayanja.

Alisema Coastal itapambana kuhakikisha wanafanikiwa kufuta uteja wa kufungwa michezo yote miwili kwenye ligi.

"Ni moja ya sababu ya mchezo huu kuwa mgumu, Coastal hawatakubali kupoteza mchezo kwa mara ya tatu kwetu, hata hivyo tumejipanga kushinda," aliongezea kusema Mayanja.

Yanga, Azam na Mwadui FC tayari zimeshafuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kuzifunga Ndanda FC, Prisons na Geita Gold Mine katika hatua ya robo fainali.