Akizungumza na gazeti hili jana, Julio alisema kuwa hana hofu yoyote na Ndanda FC ambao katika mechi yao iliyopita 'waliwakamata' Azam FC na kutoka nao sare ya 2-2.
Julio alisema kuwa licha ya kucheza ugenini amewataka Ndanda FC wasitegemee mteremko katika mchezo huo.
"Mpira ni dakika tisini, lakini mimi nasema tumejiandaa na hatuna shaka na Ndanda, tutapambana kwenye uwanja wao kwa ajili ya kupata ushindi," alisema Julio.
Mechi nyingine zitakazofanyika leo ni kati ya African Sports dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwakaribisha Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.










