Simba, Namungo vinara wa penalti

17Dec 2023
Adam Fungamwango
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Simba, Namungo vinara wa penalti

Timu za Simba na Nammungo ndizo timu zilizobahatika kupata penalti nyingi mpaka sasa kwenye Ligi Kuu, kila mmoja akipata tatu.

Baada ya kupata penalti Ijumaa katika mechi dhidi ya Kagera Sugar ikiwekwa wavuni na kiungo mshambuliaji wa Simba Saido Ntibazonkiza, Simba kwa sasa imefikisha penalti tatu huku zote zikiwa zimeweka kwenye kamba.

Saido amefunga penalti mbili ya kwanza ikiwa ni Oktoba 5, Uwanja wa Sokoine Mbeya, timu yake ilipocheza dhidi ya Prisons na kushinda mabao 3-1.

Penalti moja ya Simba ilifungwa na Jean Baleke, Septemba 21 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam dhidi ya Coastal Union, iliposhinda mabao 3-0.

Namungo nayo imebahatika kupata penalti tatu, lakini yenyewe ikikosa moja na kupata mbili ambazo zilifungwa na Derrick Mukombozi na Fabrice Ngoyi, huku Mukombozi akikosa moja.

Yanga inafuatia ikiwa imebahatika kupata penalti mbili, zote zikiwekwa wavuni.

Pacome Zouazoua alifunga penalti katika mechi ambayo katika mechi ambayo Yanga iliichabanga Simba mabao 5-1 Jumamosi iliyopita, Stephane Aziz Ki alifunga moja dhidi ya Mtibwa Sugar, ikishinda mabao 4-1.