Michuano hiyo itakayofanyika kwa mara ya pili mwaka huu, inaandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na Simba imeshathibitisha kushiriki.
Taarifa iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Nchini (TFF) inaeleza kuwa mashindano hayo hushirikisha ya timu zilizoshika nafasi ya tatu kwenye ligi. Mwaka juzi Tanzania Bara iliwakilishwa na Mbeya City ya Mbeya.
Bingwa michuano atanyakua Sh. milioni 60, wakati mshindi wa pili ataondoka na Sh. milioni 40 na mshindi wa tatu Sh. milioni 20.
Timu ya Vitoria University ya Uganda ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo.










