Baada ya kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mkwawa Queens, Lukula alisema uamuzi wa kumpa kila mchezaji nafasi ya kucheza kunasaidia kuwapa mapumziko nyota wengine na kurejesha viwango vyao wanaporudi dimbani.
"Kila mtu anapata nafasi ya kucheza, wengine wanapumzika hata mechi mbili, ukiwarudisha tena uwanjani unaona viwango vyao vinakua vikubwa, msimu huu nimempa kila mchezaji nafasi ya kucheza, hata makipa wote watatu tumegawana mechi za kucheza," alisema Lukula.
Aliongeza ligi ya msimu huu bado ni ngumu na wamejipanga kuendelea kupambana kushinda kila mechi wanayocheza.
Katika mechi hiyo ya juzi, Mkenya Shikangwa alifikisha mabao 13 na kukaa kileleni baada ya kufunga magoli mawili, Vivian Corazone na Zainabu Mohamed, wakifunga pia.










