Hadi robo ya kwanza inamalizika, Savio walikuwa mbele kwa vikapu 18-8 na waliendelea kupeta na kumaliza nusu ya kwanza wakiwa mbele kwa vikapu 18-16. Mabingwa hao waliendelea kutawala mchezo katika robo ya tatu na kufanikiwa kuongoza kwa 49-33.
Kwa upande wa wanawake, timu ya DB Lioness, walichakazwa JKT kwa vikapu 63-62 na kutwaa yati la michuano hiyo.
Mchezaji bora wa mashindano alikuwa Endrigo Augastine kutoka JKT, wakati mchezaji bora upande wa wanaume alikuwa Alyoce Komba wa Savio.
Aidha, Amiri Tambwe alitwaa tuzo ya mzuiaji bora. Kila mmoja alizawadia kiasi cha Sh. 100,000.
Washindi walizawadiwa vikombe na vyeti.










