AS Roma yamtimua Kocha Mourinho

16Jan 2024
Nipashe
AS Roma yamtimua Kocha Mourinho

KLABU ya AS Roma imetangaza kuachana na Kocha Jose Mourinho pamoja na benchi la ufundi kufuatia mwenendo mbaya kwenye Serie A.

Roma imepoteza michezo mitatu mfululizo ya Ligi Kuu ya Italia ‘Seria A’, huku wa mwisho ikiwa ni kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa AC Millan.

Kocha huyo amefanikiwa kutwaa kombe na UEFA Europa Conference League msimu wa 2021/22 akiwa na timu hiyo.

Mourinho alipewa mikoba ya kuinoa Roma Mei 2021, chini ya mwezi mmoja baada ya kutimuliwa na Tottenham Hotspur. Aliiongoza klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya sita katika misimu miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa Sportitalia, nahodha wa zamani wa Roma, Daniele De Rossi, ambaye alikuwa akiinoa SPAL, ndiye anayepewa nafasi kubwa kuchukua nafasi ya Mourinho.

Roma kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya tisa na pointi zake 29 baada ya kucheza mechi 20.