Niyonzima alicheza kwa kiwango cha juu katika mechi ya kwanza kati ya timu hizo ambayo Yanga walishinda 2-1 kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali Jumamosi.
Akizungumza na Nipashe jijini jana, Niyonzima (26), alisema amejipanga kucheza kwa kiwango cha juu tena keshokutwa dhidi ya timu yake ya zamani.
Kiungo huyo alisema anaipenda APR kwa sababu ndiyo timu iliyomlea, lakini kwa sasa anajali zaidi maslahi yake ndani ya Yanga.
"Yanga kwanza, nilikuwa APR, lakini sasa ni mchezaji halali wa Yanga," nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) alisema huku akiwataka Wanyarwanda wenzake wamsamehe kutokana na matokeo mabaya ya timu yao (APR) dhidi ya Yanga.










