Akizungumza moja kwa moja kutoka Angola na kituo kimoja cha redio hapa nchini jana asubuhi, Msuva alisema wametumia nguvu nyingi kutinga hatua ya makundi dhidi ya wapinzani wao hao.
"Mchezo ulikuwa mgumu na mbaya zaidi mwamuzi alichangia kuufanya mchezo kuwa mgumu upande wetu. Tumefanya kazi kubwa," alisema Msuva.
Aliongeza: "Nimefurahi sana kusonga mbele, itakuwa mara yangu ya kwanza kushiriki michuano ya Afrika hatua ya makundi. Hii ni historia kwangu."
Alisema kwa sasa wanafikiria kucheza hatua ya makundi kwa kujiandaa vizuri. Hatua ya robo fainali inatarajia kuanza baada ya kupangwa kwa droo Mei 24 mwaka huu.
Pamoja na Yanga kufungwa goli 1-0 kwenye mchezo huo wa juzi, Yanga wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 baada ya ushindi wa magoli 2-0 nyumbani zaidi ya wiki mbili zilizopita.










