Ivan Rakitic aliwapa uongozi wa mechi Barcelona katika dakika ya 22 kabla ya Messi kuyafanya matokeo kuwa 2-0 baada ya kugongeana vyema na Neymar dakika saba kabla ya nusu saa ya mchezo.
Diego Llorente alitolewa kwa kadi nyekundu kabla ya mapumziko baada ya kucheza rafu dhidi ya Rakitic kisha Messi akaongeza la tatu dakika 53 akimalia mpira wa Luis Suarez uliogonga nguzo, lakini Manucho akawapoza wenyeji akiitendea haki kazi nzuri ya Bebe.
Manuel Iturra alitolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili kabla ya Suarez kukosa penalti iliyotokana na kosa la mchezaji huyo, lakini Arda Turan akaongeza bao la tano la Barca.
Goli la dakika ya 72 lililokuwea la nne kwa Barca juzi usiku, lilimfanya Messi aongeze idadi ya 'hat-trick' na sasa ana magoli 20 katika mechi 16 zlizocheza mwaka huu. (Marca)










