Timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL), imeweka rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haishiriki Ligi Kuu iliyotinga robo-fainali ya Kombe la FA ikiungana na Azam FC, Coastal Union, Mwadui FC, Ndanda FC, Prisons, Simba na Yanga.
Na katika kuthibitisha kwamba hawajabahatika, Matola alisema jana kuwa sasa wako kwenye maandalizi kabambe kuhakikisha wanashinda mechi inayofuata na kutinga nusu-fainali na kwamba vijana wake "wana njaa ya mafanikio".
“Vijana wangu wananipa kiburi cha kuzungumza na kutamba kutokana na viwango vyao vizuri wanavyoonyesha katika kila mchezo tunaoshuka dimbani, wote tuna kitu na ndoto za mafanikio msimu huu, tuko kikazi zaidi, ” alisema Matola.
Kocha huyo wa zamani wa Simba pia alizungumzia tuhuma za upangaji matokeo katika mechi yao ya mwisho ya Kundi C la FDL waliyoshinda 8-0 dhidi ya JKT Kanembwa mjini Kigoma akieleza kuwa "Mungu anajua" na anaviachia vyombo vya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuamua hatima ya timu.










