Mayanja amesema kwamba asiyeamini hilo atajiridhisha Jumamosi Uwanja 2wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya watani hao wa jadi.
Mayanja amesema Kessy ni mahiri kwa kupandisha mashambulizi na kuzuia mashambulizi ya timu pinzani, kuliko hata alivyokuwa akifanya Nsajigwa enzi zake Yanga SC, kabla ya kustaafu mwaka 2013.
Pamoja na hyo, Mayanja amempa heshima yake Nahodha wa zamani wa Tanzania; “Nsajigwa alikuwa mchezaji wa kipekee Tanzania kwa miaka ya nyuma, wakati huo akicheza timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Yanga, kutokana na jinsi alivyokuwa akipandisha mashambulizi na kuzuia, lakini ninachokiona kwa Kessy hivi sasa ni zaidi ya kile alichokuwa akifanya Nsajigwa,”.
“Kessy ana kasi kubwa na ni mwepesi, lakini pia anacheza soka la kisasa, ambalo kwa sasa limetawala kote duniani. Nina imani kuwa atadhihirisha ubora wake dhidi ya Yanga Jumamosi.
Mtahitaji tu kuangalia anavyopiga krosi, pasi za haraka, lakini pia anavyokaba vizuri pale timu inapokuwa inashambuliwa,” alisema kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar na Coastal Union.
Kwa sasa, Nsajigwa ni kocha wa timu ya vijana ya Yanga, maarufu kama Yanga B, wakati Kessy ndiye beki tegemeo wa kulia wa Simba.









