Max atamba Yanga kufika mbali Afrika

30Aug 2023
Adam Fungamwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Max atamba Yanga kufika mbali Afrika

WINGA wa Yanga, Max Nzengeli Mpia, amesema kwa kikosi alichokikuta Yanga, ana uhakika watafika mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku mwenyewe akijiandaa kuipa mafanikio klabu hiyo ili kurudia kilichofanywa msimu uliopita.
Akizungumza jiji Dar es Salaam, Max jana, raia huyo

WINGA wa Yanga, Max Nzengeli Mpia, amesema kwa kikosi alichokikuta Yanga, ana uhakika watafika mbali kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku mwenyewe akijiandaa kuipa mafanikio klabu hiyo ili kurudia kilichofanywa msimu uliopita.

Akizungumza jiji Dar es Salaam, Max jana, raia huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pia amefichua siri ya kupenda kuchomekea jezi, akisema babu yake ambaye alikuwa mtanashati sana alipenda kuchomekea kila anapoonekana.

"Yanga tuna kikosi kizuri na kocha wetu amekuwa akikibadilisha kwa ajili ya kuwafanya wachezaji wote wacheze ili wawe kwenye ubora unaofanana, tuna timu ambayo nina uhakika itafanya vizuri huko mbele ya safari, sisi wachezaji wapya tuna deni ambalo ni kujitahidi na kuhakikisha tunapambana kwa sababu kama msimu uliopita timu ilifika fainali ya Kombe la Shirikisho, basi msimu huu sisi tunatakiwa tufanye vema kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, tufike mbali ili turudie kile ambacho wenzetu walikifanya huko nyuma," alisema mchezaji huyo ambaye pia kuna wakati uwanjani hucheza kama kiungo mshambuliaji.