Malinzi akemea migogoro ya uongozi

02Apr 2016
Nipashe
Malinzi akemea migogoro ya uongozi

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezitaka klabu nchini kuacha tabia ya kugombana pale fedha za wadhamini zinapoingia.

Jamal Malinzi

Malinzi alisema hayo juzi, Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye hafla fupi iliyoziunganisha Kampuni ya Acacia na Sunderland FC ya Uingereza zilizokubali kuchangia fedha za kuinua soka la Tanzania.
Malinzi alisema kitendo cha viongozi kutofautiana husababisha wadhamini kukimbia.

"Hili naomba mlisikie nyie Stand United kwa sababu mko hapa na hawa ni wadhamini wenu, mnapofanya hivyo mnawakimbiza," alsiema Malinzi.

Alisema wadhamini siku zote hupenda kuwekeza fedha zao sehemu ambazo wanajua zitawasaidia kujitangaza.
"Kwenye migogoro ya viongozi, wadhamini hawezi kuwekeza fedha zao, hivyo ili kuepuka kukosa wadhamini, lazima viongozi kufanya kazi kwa wele," alisema Malinzi.

Alizitaka klabu kujenga tabia ya kuheshimu wadhamini hao na kutekeleza makubaliano waliyoingia kwa faida ya mchezo wa soka na klabu husika.