Katika taarifa ya FIFA, imesema mechi zitakazochezwa Amerika Kusini, itakuwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 100 ya Kombe la kwanza la Dunia nchini Uruguay. Morocco itakuwa taifa la kwanza la Afrika Kaskazini kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.
Mchanganuo wa mpango huo unaonyesha kwa upande wa Afrika mechi zitachezwa katika nchi ya Morocco huku katika bara la Ulaya zitachezwa katika nchi za Hispania na Ureno na bara la Amerika Kusini mechi zitafanyika Argentina, Paraguay na Uruguay.Hata hivyo, mpango huo bado unaonekana kutoungwa mkono na baadhi ya wadau wa soka katika mitandao ya kijamii.









