BetPawa yazindua programu kuwawezesha watanzania 20 kutimiza ndoto zao

02Oct 2023
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
BetPawa yazindua programu kuwawezesha watanzania 20 kutimiza ndoto zao
  • Ni kupitia awamu ya pili ya  'Dream Maker'

Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya BetPawa Tanzania, leo imezindua awamu ya pili ya programu yake ya kuwasaidia Watanzania wenye mawazo chanya kutimiza ndoto zao inayojulikana kama ‘Dream Maker’

Afisa Mkaguzi Mkuu wa bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya dream Maker Season 2 inayoendesha na BetPawa Tanzania Dar es Salaam jana. PICHA: IMANI NATHANIEL

Kupitia awamu ya pili ya programu hiyo, jumla ya Watanzania 20 wenye mawazo ya miradi yenye uwezo wa kubadilisha maisha yao na jamii inayowazunguka, watashikwa mkono na BetPawa na hivyo kutimiza ndoto zao.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili, Meneja Masoko wa BetPawa Tanzania Borah Ndanyungu, amesema programu hiyo itahusisha mikoa mitatu ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma.

“Watu watakaokutana na basi maalum la Dream Maker watakaribishwa kupanda na kujaza form pamoja na kurekodi video kuhusu ndoto zao. Wengine ambao hawatapata fursa ya kukutana na basi, wanaweza kufanya hivyo popote pale walipo na kutuma kwa njia ya mtandao kwa kutumia hastag #betPawaDreamMaker,” amefafanua

Meneja Masoko wa BetPawa TanzaniaBorah Ndanyungu, akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya dream Maker Season 2 inayoendesha na BetPawa Tanzania Dar es Salaam jana. PICHA: IMANI NATHANIEL

Kwa mujibu wa BetPawa Tanzania, msimu wa kwanza wa Dream Maker uliofanyika Septemba 2021, uliwezesha ndoto za Watanzania 13 kutimizwa. Ndoto hizo ni pamoja na ujenzi wa nyumba mpya, viwanja vya michezo ufunguzi wa biashara mpya ambazo pia zimetengeneza ajira kwa jamii inayozizunguka. Mwaka huu, jumla ya miradi 20 itapata ufadhili.

Borah ameeleza kuwa fursa ipo wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea na kuwataka wote wenye mawazo ya miradi kujitokeza na kuyawasilisha kwa BetPawa.

“Tunafanya ubashiri kuwa rafiki zaidi kwa kuwapa watu fursa ya kubashiri kwa dau dogo na kushinda kikubwa kisha kutimiza ndoto zao. Hata hivyo, katika programu hii ya Dream Maker, huhitaji kubashiri kabisa kwa kuwa ni ya kila mtu mwenye umri wa miaka 18 au zaidi. Tueleze ndoto yako bila kujali ukubwa wake. na sisi tutakusaidia kuitimiza na kukufanya kuwa mmoja kati ya wanufaika 20 wa msimu wa pili,” alifafanua Borah 

Ameongeza kuwa BetPawa itatembelea mikoa hiyo mitatu na magari ya matangazo yatakuwa yakihamasisha watu kujitokeza na kuelezea ndoto zao. Zoezi hili litafanyika katika mikoa tofauti tofauti kila msimu hadi litakapomaliza nchi nzima.

“Lengo la BetPawa Tanzania ni kutoa fursa kwa kila Mtanzania kutimiza ndoto yake,” ameongeza