Matokeo hayo yaimefanya Simba kufikisha pointi 36 baada ya kushuka dimbani mara 16 ikishika nafasi ya tatu mbele ya Azam FC wanaoongoza msimamo na Yanga iliyopo nafasi ya pili.
Matola amesema licha ya kucheza vizuri na kumiliki mpira, bado walikuwa na makosa kwenye kujilinda hasa wakiwa wanakwenda kushambulia kwa mpinzani wao.
"Ni matokeo ya mpira, tumecheza vizuri lakini makosa ya mabeki wetu yametugharimu, tunaenda kufanyia kazi makosa yetu na kurejea kwenye ubora wetu, tulitengeneza nafasi nyingi tumeshindwa kuzitumia na wenzetu wamepata nafasi chache wamezitumia, tunawapongeza," amesema Matola.
Matola amesema kupoteza mchezo huo sio mwisho wa mapambano na kwamba bado wanamichezo mbele yao hivyo lazima warejee haraka kwenye hali yao ili kuweza kupata ushindi kwenye michezo hiyo.
Baada ya mechi ya juzi Simba sasa itasafiri kwenda Tanga kukabiliana na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakani kesho Jumamosi.
Halafu watarejea tena Morogoro kucheza na Mashujaa ikiwa mfululizo wa michezo minne ya Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kugeukia mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika.
Shirikisho la Soka Afrika, CAF, linatarajiwa kuchezesha droo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika machi 12 ambapo Simba huenda ikakutana na timu mojawapo kati ya Mamelod Sundowns, Petrol Atletico de Luanda au Al Ahly.
Michezo ya mkondo wa kwanza wa michuano hiyo inatarajiwa kucheza kati ya Machi 29 na 30 mwaka huu mbapo Simba itaanzia nyumbani.