Kazimoto ambaye kwa mara ya kwanza alitua Simba akitokea JKT Ruvu, alisema jana kuwa changamoto zinazidi kuongezeka dhidi yao wakati wa lala salama kutokana na baadhi ya timu kujiimarisha ili kutwaa ubingwa na nyingine zikipambana kulikwepa jana la kuporomoka daraja. "Mzunguko wa pili unakuwa mgumu kwa sababu kila timu inapambana kushinda na kujiweka kwenye mazingira mazuri ama ya kuwa bingwa au kuepuka kushuka daraja, kwa hiyo kila mchezo ni mgumu kwa kipindi hiki," Kazimoto aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook jana asubuhi. Alisema morari ya wachezaji wa Simba imeongezeka na kila mmoja anaposhuka uwanjani, anapambana ili timu ipate pointi tatu muhimu. "Hatujakata tamaa, mechi bado zipo, tunaomba Mungu tufanye vizuri, kila mechi ni fainali kwetu, tunataka kufuta yale yaliyotokea miaka misimu mitatu iliyopita," aliongeza kiungo huyo.
Kazimoto: Umoja utaipa ubingwa Simba
04Feb 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Kazimoto: Umoja utaipa ubingwa Simba
KIUNGO mzoefu wa Simba, Mwinyi Kazimoto, amesema mzunguko wa pili wa ligi ya Bara huwa ni mgumu zaidi, lakini anaamini umoja na ushirikiano wao ndiyo utafanikisha lengo lao la kufuta rekodi mbaya ya miaka minne bila taji la Ligi Kuu.










