Kikosi cha Muingereza Stewart Hall kilipiga kambi Zambia kushiriki michuano maalum ya kimataifa iliyomalizika jana ikishirikisha timu nne (pamoja na Zesco ya Zambia na mabingwa wa Zimbabwe, Chicken Inn).
Huku akilimwagia pongezi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lililokiuka Kanuni za Ligi toleo la 2015 kwa kuiruhusu Azam FC kukacha ratiba ya Ligi Kuu na kumtikia Zambia, Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba alisema jana kuwa kikosi chao kiko salama na kinakuja Tanzania 'kuwashika'.
Kawemba alitamba kuwa kikosi chao kiko vizuri na utaratibu unaofuata ni 'kupiga tu na kuchukua pointi tatu muhimu katika kila mchezo'.
“Ni pointi 12 katika mechi nne zinazofuata (dhidi ya Mwadui FC, Coastal, Mbeya City na Tanzania Prisons), ni kitu kinachowezekana na hiyo ni dhamira yetu na hatuna rekodi mbaya tunapocheza ugenini,” Kawemba alikaririwa katika mtandao rasmi wa Azam FC jana.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu wa 2013/14 wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa VPL wakiwa na pointi 39 baada ya mechi 15.
Michezo yao ya viporo imepangiwa ratiba mpya ambapo wataikabili Tanzania Prisons Februari 24 (Mbeya) na ule wa Stand United utachezwa Machi 16 (Dar).
Azam FC yazitangazia vita Simba, Yanga
04Feb 2016
Sanula Athanas
Nipashe
Azam FC yazitangazia vita Simba, Yanga
BAADA ya kukipiga dhidi ya Zanaco FC na kumaliza ziara ya mechi tatu za kimataifa nchini Zambia jana, uongozi wa Azam FC imetangaza vita ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).










