Akiwa kwenye gari lake aina ya ‘Toyota Premio’ aligongwa na gari kubwa la mizigo ambalo linadaiwa kutokomea kusikojulikana, lakini straika huyo hakuumia mbali na gari hilo kuharibika vibaya. Akizungumzia kilichotokea, alisema wakati anakata kona kwenye ‘round about’ ya Kijichi na Mbagala kuelekea mjini, ndipo alipogongwa na gari kubwa la mizigo ambalo lilitokomea haraka. “Kisheria inatakiwa wale wanaotoka Mbagala watusubiri sisi tunaozunguka tupite, lakini dereva wa gari hilo hakusimama akapita kwa kasi na kugonga gari langu,” alisema huku akidai kuwa alilazimika kutafuta gari la kulivuta kando ya barabara kisha ndiyo aende kuwahi kwa daktari wa mifupa ambaye alikuwa na ratiba ya kukutana naye asubuhi hiyo. Straika huyo wa zamani wa Yanga alieleza kusikitishwa na ajali hiyo huku akitaka mamlaka ya usalama barabari na jeshi la polisi kubuni mbinu kali za kuwakamata wale wanaoenda kinyume cha sheria za usalama barabarani.
Kavumbagu anusurika ajalini
03Feb 2016
Lete Raha
Kavumbagu anusurika ajalini
MSHAMBULIAJI wa Azam, Mrundi Didier Kavumbangu, jana alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya akitokea kwake Kijichi akielekea hospitali ya mtaalamu wa viungo iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa matibabu ya majeraha yake yanayomuweka nje tangu mwezi uliopita.










