Lakini akasema kuwa njia pekee ya kumsaidia ili aweze kupata nafasi mbele ya Tambwe na Ngoma ni kufanya mazoezi binafsi nje ya ratiba ya kocha Hans van der Pluijm. Busungu ambaye msimu uliopita alitamba akiwa na Mgambo JKT kabla ya kusajiliwa Yanga, amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Mholanzi huyo huku mastraika Donald Ngoma na Amissi Tambwe wakizidi kupewa nafasi. Maganga alisema, “Huu ni mpira na kila kocha ana vigezo vyake linapokuja suala la nani acheze na nani akae benchi. Kwa uwezo wa Busungu inanisikitisha sana kwani ninatamani kumwona akicheza kila mara. “Kukaa kwake benchi Yanga huenda kukampoteza kama ilivyokuwa kwa straika Said Bahanuzi na Hussein Javu ambao walianza vizuri Yanga lakini baadaye wakapotezwa. Ili Busungu aweze kushindana na wachezaji wa kigeni ambao wanaonekana kuaminika zaidi ni lazima ahakikishe anafanya mazoezi yake binafsi mbali na yale anayotoa kocha. “Mazoezi binafsi kwa mchezaji humjenga na kumfanya bora zaidi ya jinsi alivyokuwa hapo awali hivyo asisite kupambana kwa kujiongezea muda wa mazoezi,” alisema Maganga. Straika huyo alicheza na Busungu na kuiongoza Mgambo kwenye mbio za Ligi Kuu msimu uliopita.
Busungu apewa mbinu za kumpoteza Ngoma
03Feb 2016
Lete Raha
Busungu apewa mbinu za kumpoteza Ngoma
NAHODHA wa Mgambo JKT, Fully Maganga, amesema kuwa anasikitishwa na hali aliyonayo straika Malimi Busungu kwenye kikosi cha Yanga.










