Kamati ya Nidhamu yamsimamisha Rais wa Shirikisho la Soka Hispania

27Aug 2023
Nipashe Jumapili
Kamati ya Nidhamu yamsimamisha Rais wa Shirikisho la Soka Hispania

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), imemsimamisha kwa muda Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini Hispania, Luis Rubiales kwa siku 90 kutokana na kitendo cha Rubiales kushika kichwa cha mchezaji Jenni Hermoso na kumbusu mdomoni baada ya ushindi kwenye Kombe la Dunia la Wanawake.

Rubiales alitarajiwa kutangaza kujiuzulu siku ya Ijumaa lakini badala yake akasema hatajiuzulu, na shirikisho la soka la Uhispania (RFEF) lilitishia kuchukua hatua za kisheria kumtetea baada ya Hermoso kusema kuwa Rubiales alimbusu bila ridhaa yake.

“Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya FIFA, ameamua kumsimamisha kwa muda bwana Luis Rubiales kwenye shughuli zote zinazohusiana na soka kwenye ngazi ya Taifa na Kimataifa,” -FIFA imesema.