Amesema kuwa kinachowaharibia baadhi ya wasanii ni kudhani kuwa wakisifiwa tu basi wameyapatia maisha na kumbe bado wanahitaji kufanya juhudi na maarifa ili kufikia kule wanakotaka badala ya kubweteka.
"Ninasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya wasanii wakipata umaarufu kidogo wanaanza nyodo na kutengeneza matabaka kitu ambacho kinawagawa wenyewe kwa wenyewe na kusahau kwamba mafanikio hayaji hivi hivi bila kujituma," amesema Mwegelo.
Amesema kuwa umaarufu wa msanii unatakiwa kwenda sambamba na ushirikiano na wengine katika kazi za sanaa na mambo mengine ya kijamii kuliko kujiona amefanikiwa na kudhani ni bora kuliko wengine wote wanaomzunguka.
"Kimsingi ni kwamba wasanii wenzangu na hasa wa muziki huu wa kizazi kipya wanpaswa kutambua kwamba mafanikio yao yanatokana na mashabiki hivyo hawana budi kuonyesha kwamba wapo hapo kutokana ushirikiano wanaopata hivyo wao washirikiane na wenzao," amesema.










