JKT Ruvu yalilia sare

19May 2016
Renatha Msungu
Dar
Nipashe
JKT Ruvu yalilia sare

TIMU ya JKT Ruvu imeingia kambini kujiandaa na mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa.

JKT Ruvu

Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa timu hiyo Costantine Masanja alisema mchezo huo wanahitaji kushinda ili kukwepa kushuka daraja.

Masanja alisema kwamba wanatarajia kutumia nguvu za ziada ili kuhakikisha wanapata pointi tatu na kusalimika kuifuata Coastal Union ya jijini Tanga.

"Msimamo wa ligi ulivyo unatufanya tuwe na tahadhari kubwa, hata sare kwetu itatusaidia, endapo tutapoteza mechi na timu nyingine zilizo chini zikishinda, tutakuwa matatani," alisema Masanja.

JKT Ruvu iko katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 29 na salama yake ni kuifunga Simba au timu zilizoko chini yake ambazo ni African Sports, Mgambo Shooting na Kagera Sugar zifanye vibaya.