Kwa mujibu wa takwimu za Ligi Kuu, Simba inaongoza kwa kuwa na 'hat-trick' nyingi zaidi ikiwa nazo nne, huku wachezaji wake wakiongoza pia.
Timu hiyo ina wachezaji watatu waliofunga hat-trick hizo ambao ni nahodha, John Bocco, Saido Ntibazonkiza na Jean Baleke.
Bocco ndiye mchezaji aliyefunga hat-trick mbili msimu huu, huku Ntibazonkiza na Baleke wakifunga moja.
Jumamosi iliyopita, straika raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Baleke alifunga 'hat-trick' yake ya kwanza tangu atue nchini wakati Simba ikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar na kupata ushindi wa mabao 3-0.
Straika wa Yanga, Fiston Mayele yupo kwenye orodha ya wachezaji waliofunga mabao matatu kwenye mechi moja, akifanya hivyo Desemba 20, mwaka jana kwenye mechi dhidi ya Singida Big Stars iliyomalizika kwa mabingwa hao watetezi kupata ushindi wa mabao 4-1.
Januari 23 mwaka huu, straika wa Namungo FC, Ibrahim Mkoko aliingia kwenye orodha ya wapiga hat-trick katika ligi hiyo wakati walipowavaa KMC na timu yake kumaliza mechi kwa ushindi wa mabao 3-1.










