Hanspoppe alianzisha tena Yanga

14Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Hanspoppe alianzisha tena Yanga

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amewaponda wapinzani wao, Yanga kwamba hawana lolote kuelekea mchezo baina ya miamba hiyo ya soka nchini, wiki ijayo.

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amewaponda wapinzani wao, Yanga kwamba hawana lolote kuelekea mchezo baina ya miamba hiyo ya soka nchini, wiki ijayo.

Simba na Yanga SC zitamenyana katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumamosi wiki ijayo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Hans Poppe amesema watawaangusha mahasimu wao hao siku hiyo.

Akizungumza na Lete RAHA juzi, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), alisema kwamba Yanga wanatapatapa na wanapumulia mashine kwa sasa, hivyo wategemee kumalizwa na Simba katika mechi yao ya Ligi Kuu Jumamosi ijayo.

“Furaha ya kuwanyoa Yanga ni mara tatu ya furaha ya kawaida, kwani kipigo wanachopata watani wetu hao katika soka ni sherehe tosha kwa Simba, haswa kwa mbwembwe za mashabiki wetu,” alisema Hans Poppe.

Ikumbukwe mchezo wa kwanza mwaka jana, Simba SC ilichapwa 2-0 mabao ya Malimi Busungu na Amissi Tambwe na Jumamosi ijayo watakuwa na deni la kulipa.