Cheka ‘akata kilo nane’ kupata wepesi wa kumtwanga Mzungu

24Feb 2016
Lete Raha
Cheka ‘akata kilo nane’ kupata wepesi wa kumtwanga Mzungu

BONDIA Francis Cheka, amepunguzauzitowakilogramunanekutokananamazoezimakalikujiandaanapambanodhidiyaMuingerezamwenyeasiliya Serbia, GeardAjetovivlitakalofanyikaJumamosikwenyeviwanjavya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam kuwaniaubingwawaMabarawa WBF uzitowa Super Middle.

Akizugumza na LeteRaha Cheka ambaye anaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Mango baada ya awali kuweka kambi ya wiki tatu Zambia, amesema kwamba alianza mazoezi chini ya kocha Saleh Abdallah akiwa ana uzito wa kilogramu 84, lakini sasa zimepungua hadi kubaki 76.

“Nina kila sababu ya kuhakikisha nafanya vizuri kwenye mchezo huo, ni pambano kubwa na hitaji kushinda,”,alisema Cheka.
Akizungumzia upande wa maandalizi kwa ujumla alisema yanaendelea vizuri kutokana na kwamba yuko kwenye hatua za mwisho za maandalizi ya pambano hilo.

Promota wa pambano hilo, Jumanne Msangi, alisema majaji na waamuzi wapambano hilo, wanatarajia kuwasili leo (Jumatano), tayari kwa pambano hilo.

Msangi alisema ugeni huo, utakapo wasili nchini, moja kwa moja utakwenda kuonana na Waziri wa Habarani Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nanauye ambaye anaamini watajadiliana kuhusiana na kupandisha mchezo wa ngumi.