Wagombea watano (hakuna kutoka Afrika), watajipanga jukwaani kujinadi, kisha kupigiwa kura.
Ni pamoja na Prince Ali bin al-Hussein, Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne.
Uchaguzi huo unakuja kutokana na uamuzi wa rais aliyetangulia Sepp Blatter aliyedumu kwenye nafasi hiyo yangu mwaka 1998, kujiondoa madarakani kutokana na tuhuma za rushwa.
Itakuwa mara ya kwanza Fifa kufanya uchaguzi na kupata sura nyingi mpya, lakini kubwa ni nafasi ya urais iliyokuwa ikishikiliwa na mtu mmoja kwa miaka 18 mfululizo.
Sheikh Salman na Infantino, kila mmoja ana nafasi nzuri ya kupata urais kwenye shirikisho hilo lenye dhamana ya kusimamia mchezo wa soka.
Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) aliyesimamishwa, Michel Platini kubwa ya kushinda, lakini yeye pamoja na Blatter wamepigwa stop kujihusisha na soka kwa miaka sita kwa tuhumu za rushwa.










